You are currently viewing STIVO THE SIMPLE BOY ATHIBITISHA KUWA MGONJWA, AANDIKA UJUMBE MZITO INSTAGRAM

STIVO THE SIMPLE BOY ATHIBITISHA KUWA MGONJWA, AANDIKA UJUMBE MZITO INSTAGRAM

Msanii wa muziki nchini Stephen Otieno maarufu kama Stivo The Simple Boy amewaacha mashabiki na maswali mengi baada ya kuchapisha ujumbe kwenye akaunti yake mpya ya Instagram akisema kwamba amekuwa mgonjwa kwa muda sasa.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mihadarati” ameposti picha akiwa kwenye mazingira ya studio yenye caption inayosomeka “Mziki ni dawa yangu, Mafans wangu wish me a quick recovery niwapee ngoma mpya. Au sio.”,  ujumbe unaowataka mashabiki zake wamuombee apate nafuu ili aweze kuwabariki na ngoma mpya.

Posti yake hiyo imeibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki zake ambao walishuka kwenye uwanja wa comment ya post kwenye mtandao wa Instagram na kumtakia afueni ya haraka.

Stivo The Simple ni miongoni mwa wasanii wachache ambao wamewakosha wapenzi wa muziki mzuri nchini Kenya kutokana na aina ya uimbaji wake lakini pia ni moja kati ya wasanii waliopata umaarufu mkubwa ndani ya kipindi kifupi tofauti na wasanii wengine.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke