Wimbo wa Sukari kutoka kwa mwanamuziki Zuchu umeshika nafasi ya kwanza katika orodha ya nyimbo 10 zilizo tazamwa zaidi nchini Kenya katika mtandao wa youtube.
Wimbo huo uliopandishwa katika mtandao wa YouTube Januari 10, mwaka huu pia unashikilia rekodi ya kuwa miongoni mwa nyimbo zilizo tazamwa zaidi Barani Afrika kwa mwaka 2021, ukiwa na zaidi ya watazamaji million 61 katika mtandao wa Youtube.
Mbali na Zuchu pia wimbo wa Baikoko wa Mbosso na Diamond Platnumz umeshika nafasi ya pili, ambapo ni wasanii wa 3 tu kutoka Tanzania akiwemo muimbaji wa nyimbo za injili Rose Muhando waliotokea katika orodha hiyo ya nyimbo 10 zilizo tazamwa zaidi nchini Kenya kwa mwaka 2021.