You are currently viewing SUSUMILA AKANUSHA KUSTAAFU MUZIKI

SUSUMILA AKANUSHA KUSTAAFU MUZIKI

Msani nyota nchini Susumila amekanusha kustaafu muziki baada ya kuonekana kutokuwa na mazoea ya kuachia kazi mfululizo bila kupoa kama kipindi cha nyuma.

Akizungumza na Captain Nyota Susumila amesema madai hayo sio ya kweli huku akisisitiza kuwa ataendelea kufanya muziki hadi mwisho wa dunia.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Siasa duni” amesema kwa sasa ashindani na msanii yeyote kwa kuwa tayari ana jina kwenye tasnia ya muziki nchini Kenya, hivyo ataachia nyimbo zake bila kushurutishwa na mtu yeyote.

Sanjari na hilo Susumila ambaye amekaa kwenye tasnia ya muziki nchini kwa kipindi cha miaka 15, amedokeza ujio wa kolabo yake na staa kutoka Nigeria Davido kwa kusema kuwa kwa sasa wanaendelea na mazungumzo kufanikisha kolabo hiyo.

Utakumbuka Susumila juzi kati alidai kuwa ataachia kazi yeyote ya muziki wakati huu taifa la Kenya linaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 kwa sababu ya wimbi la siasa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke