Januari 15 mwaka wa 2020 Staa wa muziki nchini Susumila alitubariki na singo inayokwenda kwa Sonona akiwa ameshirikisha msanii wa Bongofleva Mbosso.
Goods news ni kwamba Wimbo huo umefanikiwa kufikisha jumla ya streams millioni 1.5 kwenye mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa Boomplay Kenya.
Licha ya wimbo wa Sonona kufanya vizuri kwenye mtandao wa Boomplay,wimbo pia unazidi kupata mapokezi mazuri kwenye mtandao wa youtube kwani ndani ya kipindi cha miaka miwili imefanikiwa kutazamwa zaidi ya mara millioni 13.8 kwenye mtandao huo.
Ikumbukwe Sonona ni singo ya kwanza kwa mtu mzima Susumila kufanya kazi na msanii wa lebo ya muziki ya WCB, ya pili ilikuwa ni Warembo wa Mombasa aliyomshirikisha Lava Lava.