Mwanamuziki mashuhuri nchini Suzanna Owiyo ameikashifu Serikali ya Kaunti ya Kisumu na Wizara ya Ugatuzi kwa madai ya kususia kuwalipa wasanii waliotumbuiza katika Kongamano la Tisa la Africities, lililofanyika jijini Kisumu kuanzia tarehe 17 hadi 21 Mei mwaka 2022.
Kwa mujibu wa Suzanna, licha ya kuwasilisha lalama zake kwa waandaaji wa kongamano hilo wameingiwa na jeuri kiasi cha kutochukua simu zake kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa.
Hata hivyo kutokana na wasanii hao kumdhulumiwa haki yao, ametoa wito kwa Serikali ya Kaunti ya Kisumu pamoja na Serikali ya Kitaifa, kuheshimu mikataba yao na kuwalipa fedha zao.