You are currently viewing SUZZANA OWIYO AWAPA SOMO WATOTO WA KIKE

SUZZANA OWIYO AWAPA SOMO WATOTO WA KIKE

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Suzanna Owiyo ametoa changamoto kwa watoto wa kike kuanza kuthamini miili yao jinsi ilivyo badala ya kujaribu kubadilisha mienekano yao kwa kutumia madawa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Owiyo ameonesha kusikitishwa na kuongezeka kwa visa vya watoto wa kike nchini kubadilisha miili yao kuendana na nyakati zilizopo kwa kuwataka wajitenge na masuala ya kutumia vipodozi vya kubadilisha nyuso zao na makalio kwa kuwa zina athari kubwa katika maisha yao.

“Young ladies; SUZANNA Wewe umekataa kuzeeka!!… when you start appreciating your butts, Big/Small/ Flat.  What’s with the fake butts anyway! Fake butt pads, butt silicone, buttocks shaper panty… blah blah,” Aliandika Instagram.

Hitmaker huyo wa ngoma ya Ng’ato Gi Mare’ amewashauri watoto wa kike kuacha kasumba ya kujipa shinikizo zisizo na msingi za kutumia vipodozi hatari vya kujichubua kupendeza na badala yake waanze kujipenda kwa kuthamini maumbile yao kwa kuwa miili yao ni vitu vya dhamana walivyozawadiwa na Mwenyezi Mungu.

“ Acheni kujipatia stress haziko. Gels! Learn to love & embrace your body. It’s the most amazing thing you”ll ever own,”  “Stop stressing yourself with non-existent things. Gels! Learn to love & embrace your body…Call me Analogue but Fake b*** issa NO,”  Caption yake imesomeka.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke