You are currently viewing SYLVIA SSARU ATANGAZA UJIO MPYA MWAKANI

SYLVIA SSARU ATANGAZA UJIO MPYA MWAKANI

Wakati tukielekea ukingoni kabisa mwa mwaka 2021, na kuukaribisha mwaka 2022, Female rapper kutoka Kenya anayetajwa kuwa na sauti ya kipekee yenye uwezo wa kumtoa nyoka pangoni, mwanadada Sylvia Ssaru ameweka wazi kuwa  mwakani ataachia album yake mpya.

Lengo Ssaru ni kukata kiu ya mashabiki wake ambao wanatamani kuisikia sauti ya mwimbaji huyo hodari nchini  ikiwapa burudani ya kipekee.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kuipokea album yake mpya ambayo kwa mujibu wake itatoka rasmi mwanzo kabisa mwa mwaka mwa.

Lakini pia amedokeza kwamba mwaka wa 2022 atakuwa moja kati ya wasanii watakaosainiwa na lebo ya seven hub creative ambayo inamsimamia msanii nadia mukami.

Sylvia Ssaru ametoa taarifa hiyo mara baada ya kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wamempa kwenye muziki wake na kufanya kuwa miongoni mwa wasanii wa kike waliosikilizwa zaidi nchin kwenyew mtandao wa BoomPlay Kenyalicha ya kutoachia kazi nyingi mwaka huu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke