You are currently viewing TAMASHA LA NYEGE NYEGE LARUHUSIWA KUFANYIKA UGANDA

TAMASHA LA NYEGE NYEGE LARUHUSIWA KUFANYIKA UGANDA

Hatimaye tamasha la kila mwaka la burudani liitwalo “Nyege Nyege” la nchini Uganda limeruhusiwa kufanyika baada ya Bunge la nchini humo kuagiza kusitishwa kufuatia madai ya uchochezi wa uasherati.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Uganda, waandaaji wa “Nyege Nyege” wameruhusiwa kuendelea na mipango yao juu ya tamasha hilo na limetakiwa kufanyika kwa kuzingatia taratibu mpya walizopewa.

Tamasha la “Nyege Nyege” 2022 linatarajiwa kufanyika wiki ijayo mjini Jinja, kwa siku nne mfululizo kuanzia Septemba 15.

Usemi “Nyege Nyege” unamaanisha hamu isiyozuilika ya kucheza katika lugha ya Kiganda lakini pia inaweza kuwa na maana ya ngono katika lahaja nyingine za eneo hilo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke