You are currently viewing TANASHA AKANUSHA MADAI YA KUWAKIMBIA WAANDISHI WA HABARI

TANASHA AKANUSHA MADAI YA KUWAKIMBIA WAANDISHI WA HABARI

Msanii Tanasha Donna amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kuwa ameanza kuwafungia vioo waandishi wa habari wanaotaka kufanya naye mahojiano kuhusu shughuli zake za kimuziki.

Katika mahojiano na Mpasho, Tanasha amesema madai hayo hayana ukweli wowote kwani watu walitafsiri vibaya kauli yake aliyotoa juzi kati kuhusu wanablogu wa Tanzania waliomchafulia jina kwa stori za kutunga.

Mrembo huyo amesema yuko tayari kufanya mahojiano na mwaandishi yeyote wa habari ambaye ana nia njema ya kumuunga mkono kwenye harakati za kutanua wigo wa muziki wake uweze kuwafikia wengi.

Katika hatua nyingine mrembo huyo amefunguka na kudai sababu kubwa ya yeye kubadilisha aina ya uimbaji katika muziki ni kutaka kukimbizana na kizazi cha sasa na sio kubakia pale alivyokuwa awali.

Tanasha amedai suala la kubadilika ni jambo la kawaida huku akidai kuwa anachofanya kwa sasa ni kutaka kuendana na nyakati zilizopo kwani kuwa kwenye kiwanda cha muziki ambacho kina ushindani kuna hitaji msaani kuwa na ubunifu.

Tanasha Donna kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake uitwao “Karma” ambao ameufanya kwa mahadhi ya muziki wa trap.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke