Msanii kutoka Kenya Tanasha Donna amesikitishwa na taarifa ya uongo ambayo inasambaa mtandaoni kuwa Iran imetoa hukumu ya kifo kwa takriban watu 15,000 walioandamana kufuatia kifo cha Mahza Amini, binti aliyefarikiwa mikononi mwa polisi.
Kupitia video yake aliyoichapisha kwenye mtandao wa Instagram Tanasha amewataka watu kufanya dua kwa ajili ya maandamano na kinachoendelea Iran badala ya kueneza propaganda kuwa wafungwa wanawake mabikra wanabakwa kwanza kabla ya hukumu ya kifo kutolewa kwao.
Kauli yake imekuja mara baada ya Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau kupata ukosoaji mkubwa kutoka kwa serikali ya Iran mara baada ya kutumia mitandao yake ya kijamii kusema kwamba taifa hilo lilitoa hukumu ya kifo kwa watu 15,000 walioandamana kufuatia kifo cha Mahza Amini, aliyefarikiwa akiwa anashikiliwa na polisi kwa kosa la kutovalia vazi la Hijab.