Wakati mashabiki wa Staa wa muziki nchini Tanasha Donna wakiendelea kuisubiria EP kutoka kwa mrembo huyo ambayo haijulikani itatoka lini,Tanasha yeye ameamua kujiunga rasmi na tasnia ya uigizaji.
Hii ni baada ya kutajwa kuwa atakuwa mmoja wa wahusika kwenye tamthilia iitwayo Symphony ambayo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Septemba 9 mwaka 2022.
Symphony ni Tamthilia kutoka Nigeria ambayo kauli mbiu yake ni vijana na muziki.
Kutokana na taarifa za Tanasha kujiunga na tasnia ya uigizaji wakenya wengi wameonyesha kuwa na kiu ya kutaka kumuona mrembo huyo kwenye filamu hiyo ambapo wengi wamehoji kuwa huenda ni mwigizaji mkali.
Tamthilia ya Symphony imetajwa kuwa itaangazia masuala ya maisha, Mapenzi,, mafanikio, kwa kijana mwaafrika ambaye anapambana kushinda changamoto ili aweze kufanikiwa kimaisha.