Mrembo maarufu mitandaoni Risper Faith amemtuhumu msanii wa kike nchini Tanasha Donna kwa madai ya kukwepa kulipa deni la shillingi laki 8 baada ya kufanyiwa Upasuaji (Plastic Surgery) kwa ajili ya kutengeneza mwili wake.
Kulingana na Risper Faith, licha ya kampuni ya Body by Design Kenya kutoa huduma ya Plastic Surgery kwa Tanasha Donna, msanii huyo ameshindwa kulipa kampuni hiyo kwani kila mara akiulizwa kuhusu deni hilo anaingiwa na jeuri.
Kupitia ujumbe aliyoishare na mwanablogu mwenye utata Edgar Obare,Risper Faith amesikitishwa na hatua ya Tanasha kwenda kinyume na mkataba aliyoiweka na kampuni ya Body by Design Kenya ya kuchapisha huduma walizompa kupitia ukarasa wake wa Instagram.
Mrembo huyo amenda mbali zaidi na kusema kwamba Tanasha Donna amemvunjia heshima ikizingatiwa kuwa yeye ndiye alimtambulisha kwenye kampuni ya Body by Design Kenya baada ya kutaka kufanyiwa upasuaji wa kuiweka mwili wake sawa.
Ikumbukwe hii sio mara ya kwanza kwa Tanasha Donna kudaiwa kushindwa kulipa deni kwani mapema mwaka huu alidai kukwepa kulipa deni pesa ya huduma ya make up aliyopewa wakati anaaanda Video ya wimbo wake uitwao “Kalypso”.
Lakini pia mwaka wa 2020 alianikwa na baadhi ya wafanyibiashara wa nguo Jiji Nairobi baada ya kushindwa kulipa deni la shillingi 23100