Staa wa muziki nchini, Tanasha Donna ambaye kwa sasa yupo Dubai, akiwa mjini humo amekutana na mwanamasumbwi maarufu Duniani toka nchini Marekani Floyd Mayweather.
Tanasha Donna ambaye yupo Dubai kwa shughuli zake za kimuziki, amekutana na Mayweather ambaye alitua jijini humo kwa ajili ya pambano lake na Deji ndani ya Cocacola Arena mwishoni mwa wikiendi iliyoisha.
Donna ame share picha pamoja na video akiwa na mwanamasumbwi huyo kupitia Instastory yake kwenye mtandao wa Instagram.