Msanii wa kike nchini Tanasha Dona amefunguka na kudai kwamba hana muda wa kungangania penzi la mwanaume.
Kupitia ukurasa wake wa Twittwer Tanasha amejinasibu kwa kusema kwamba atokuja kulilia penzi la mwanaume katika maisha yake huku akisisitiza kuwa ikitokea amejiaibisha mbele ya umma kwa kumgombania mwanaume mashabiki zake wamuadhibu juu ya hilo.
Hitmaker huyo ngoma ya “Mood” amesema ana ufahamu mpana kuhusu suala la wanaume kuwaoa wanawake zaidi ya mmoja ila Mwenyezi Mungu anajua kwamba hatokujaa kuolewa kama mke wa pili kutokana na wivu alionao kwenye ishu ya mahusiano ya kimapenzi.
Kauli Tanasha Donna imekuja mara baada ya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kumshinikiza alipiganie penzi la Baby Daddy wake Diamond Platinumz ambaye katika siku za hivi karibuni ameonekana akiwa karibu na Zuchu ambaye anadaiwa kuwa mpenzi mpya wa hitmaker huyo wa ngoma ya “Naanzaje”.