Msanii Tanasha Donna hatimaye amethibitisha kuwa yeye na mpenzi wake aliyekuwa akisemekana ni Mzungu wameachana.
Kupitia Instagram live Tanasha amedai kuwa sababu ya kuachana kwao ni Usaliti ambapo amesema alichukizwa na kitendo cha mpenzi wake huyo kutoka kimapenzi na mwanamitindo mmoja barani ulaya licha ya kumueleza kuwa yupo single.
Tanasha donna ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya “Karma” amesema hatompa nafasi nyingine jamaa huyo kwenye maisha yake kwa kuwa hapendi kabisa watu waongo.