Nyota wa muziki nchini Tanasha Donna anaendelea kutupasha mapya kuhusu ujio wa EP yake mpya ambayo ana mpango wa kuiachia hivi karibuni.
Katika mahojiano na mpasho mkali huyo wa ngoma ya Complicationship amesema kwamba EP yake aliyoipa jina la This is me imekamilika kwa asilimia mia baada ya kuifanyia kazi kwa takriban mwaka mmoja na miezi mitatu.
Tanasha ameenda mbali zaidi na kuwahakikishia mashabiki zake kwamba watarajie kupokea EP nzuri yenye jumla ya mikwaju 5 ya moto ambayo itazungumzia safari yake ya muziki wake.
Hii ni EP ya pili kwa mtu mzima Tanasha Donna tangu aingie kwenye soko la muziki Afrika mashariki baada ya EP yake ya kwanza DONNA TELLA ya mwaka wa 2020 kufanya vizuri.