You are currently viewing TANASHA DONNA AWACHANA WANA BLOGU WA TANZANIA

TANASHA DONNA AWACHANA WANA BLOGU WA TANZANIA

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya, Tanasha Donna amechukizwa na Mablogger wanaotumia maudhui yenye utata kutoka kwa wasanii kuuza maudhui yao.

Kupitia Insta Story Tanasha amesema kuna Blogger toka Tanzania alimuomba kufanya naye mahojiano ambapo walizungumza kuhusu muziki na sanaa lakini mwisho wa siku kaenda kuandika vitu sivyo!.

“Baadhi ya Wanablog hawana heshima, Blogger wa Kitanzania alinitumia ujumbe na alikuwa akiniita katika mahojiano. Niliwapa muda wangu ili wasijisikie nina kiburi kwani wamekuwa wakijaribu kunitafuta kwa muda sasa,” alisema Tanasha.

Aliendelea kwa kusema kusema “Alinitumia maswali na kufanya ionekane kana kwamba analenga sanaa, hata kuulizwa kuhusu filamu mpya niliyoshirikishwa, kisha kuhaririwa na kuachwa sehemu ambayo itaonekana yenye utata zaidi”.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke