Msanii wa kike nchini Tanasha Donna ameamua kuanika siri za tuzo za kimataifa akidai ni za kupangwa.
Kupitia mfululizo ya posti zake kwenye mtandao wa Instagram (Instastory) amezituhumu tuzo hizo ambazo hajazitaja jina kuwa waliwahi kumpigia simu na kumtaka atoe hongo ili wamtangaze mshindi na alipokataa hakupewa tuzo.
Tanasha ambaye anafanya vizuri na single yake mpya “Karma” amewataka waandaji wa tuzo kuacha kumteua kwenye vinyang’anyiro vya tuzo hizo.
Hata hivyo hajabainika ni kitu gani kilimpelekea mrembo huyo kuibua tuhuma hizo dhidi ya tuzo za muziki.