You are currently viewing Tanasha Donna awapa somo mashabiki juu ya usafi

Tanasha Donna awapa somo mashabiki juu ya usafi

Mwimbaji wa muziki kutoka nchini Kenya, Tanasha Donna amesistiza usafi kwa wanaume na wanawake.

Tanasha amesema kwa mtu yeyote haijalishi anapitia changamoto gani katika maisha, lakini ahakikisha unanukia vizuri popote uendapo.

“Sijui ni mara ngapi tutalizungumzia hili lakini watu wangu, wanawake kwa wanaume, usafi ni kitu cha muhimu sana. Ni muhimu sana watu wangu kama hamkuwa mnajua,” Tanasha Donna alianza kushauri.

“Hakikisha unanukia vizuri si tu kwa kujirembesha kwa marashi kwa nje, lakini usafi halali. Hakikisha unanawa mikono yako, usisahau kufanya utaratibu wa kukoga kati ya mara mbili na mara tatu kwa siku, piga mswaki, tumia kopo la msalani vizuri na pia osha kwa maji baada ya kumalzia kukata gogo. Nyoa nywele zote mwilini mwako, kaa nadhifu,” alisema Tanasha.

Aliendelea kwa kusema “Natumai wengi wenu mmesikia nukuu kuwa usafi humweka mtu karibu na kumcha Mungu, ni ukweli watu wangu. Utagundua kuwa kukiwa na uchafu karibu nawe unapoteza dira ya akili lakini wakati kuna usafi unahisi mwenye utulivu na amani. Miili yetu ni hekalu takatifu la Mungu, tuilinde wote wake kwa wanaume,” Alisema.

hata hivyo mwanamuziki huyo amesema yeye hawezi kubaliana na wale wanaosema ‘mwanaume ni jasho’ huku akisema kudumisha usafi ni kwa watu wote.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke