Nyota wa muziki nchini Tanasha Donna amewatolea uvivu wamiliki wa maeneo ya burudani na waandaji wa matamasha mara baada ya tamasha lake huko Taita Taveta kukumbwa na changamoto lukuki.
Kupitia Instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Tanasha Donna ametoa ya moyoni kwa kusema kwamba aliumizwa na kitendo cha vyombo vya sauti kukwama akiwa jukwaani kwenye tamasha hilo kutokana na ubovu wa sauti jambo ambalo anadai lilimlazimu kuondoka jukwaani kabla ya muda wake haujakamilika.
Hitmaker huyo wa “Mood” amewataka wamiliki wa maeneo ya burudani na waandaji wa matamasha ya muziki kuwekeza kwenye vyombo vya sauti iwapo wanataka wasanii watumbuize kwenye matamasha yao kwa manufaa ya mashabiki na wasanii kwa ujumla.