Staa wa muziki nchini Tanasha Donna ameonyesha kusikitishwa na jinsi habari kuhusu maisha na muziki wake inavyoripotiwa.
Kupitia waraka mrefu aliyochapisha kwenye mtandao wa Instagram Tanasha Donna amesema watu wamekuwa wakiangazia sana mabaya yake propaganda badala ya kumuunga mkono kwenye muziki wake.
Mrembo huyo amewataka wanablogu na vyombo vya habari nchini kuwatangaza wasanii wa Kenya badala ya kueneza umbea ambao hauna ukweli wowote.
Hitmaker huyo wa “Gere” ametoa changamoto kwa wa Kenya kuendelea kustream nyimbo za wasanii wao wanaowapenda kama njia ya kuwasapoti.
Kauli ya Tanasha Donna imekuja mara baada ya kudaiwa kuwa alishindwa kulipa kampuni moja inayojihusisha na masuala ya surgery shillingi laki nane za Kenya baada ya kupewa huduma ya upasuaji yaani plastic surgery kuuweka mwili wake sawa