Nyota wa muziki nchini Tanasha Donna ametangaza kuachia EP yake mpya aliyoipa jina la “This is Me”
Kupitia Instagram Live mrembo huyo ameweka wazi kuwa November 12, mwaka huu ataachia wimbo wa kwanza utakaopatikana kwenye EP yake ambayo hajaweka wazi tarehe ya kutoka ila amesema kuwa itaitwa “This is Me“.
Lakini pia Tanasha amesema kuwa kupitia video hiyo ya wimbo wake wa kwanza kwenye EP amecheza sana kuliko kawaida na video ya wimbo huu imefanyika nchini Nigeria
Hii ni EP ya pili kwa mtu mzima Tanasha Donna tangu aingie kwenye soko la muziki Afrika mashariki baada ya EP yake ya kwanza Donna Tella kufanya vizuri.