Rapa Octopizzo ametangazwa kuwa balozi wa simu mpya ya Mkononi kutoka kampuni ya Tecno Kenya inayokwenda kwa jina la Tecno Spark 9 Series itakayouzwa katika maduka yote ya simu nchini.
Akizungumza na waandishi habari leo jijini Nairobi, Mkurugenzi wa Techno, Peter Shi amesema kuwa wanatarajia jamii itafaidika kwa kupata elimu kuhusu bidhaa za kampuni hiyo kupitia kwa balozi Octopizzo kwani wameamua kuileta simu ya Techno Spark 9 series ili waweze kuwasaidia wananchi wa hali ya chini kumiliki simu janja .
Kwa upande wake Rapa Octopizzo ameishukuru kampuni Techno kwa kumwamini na kutambua kuwa ana vigezo stahili kuwa balozi wao na kuahidi kuwa hatowaangusha katika kuitangaza kampuni hiyo sambamba na bidhaa zake zinazozalishwa na kampuni hiyo ambayo utengeneza simu, Kompyuta na vifaa vingine vya teknolojia
Octopizzo sasa atatakiwa kutangaza bidhaa za Techno Spark 9 Series kwa mashabiki zake kupitia mitandao yake ya kijamii kwa lengo la kuiongezea kampuni hiyo mauzo.