Akaunti ya Spotify ya Rapa Tekashi 69 kutoka Marekani imedukuliwa (Hacked) na wadukuzi.
Hii imekuja mara baada ya ghafla kubadilishwa kwa Profile Pic (DP) kwenye akaunti yake hiyo na kuwekwa picha ya Rapa Trippie Red na Lil Durk.
Sio hayo tu Bio ya rapa huyo pia imebadilishwa ambapo kwa wale waliofikia akaunti hiyo kwa muda huo walikutana na ujumbe ulioandikwa kuwa Tekashi 69 amekuwa akiishi kwa kutamani kuja kuwa kama rapa Trippie Red na Lil Durk.
Mashabiki wa Trippie Red na Lil Durk wametajwa kuhusika na udukuzi huo ikizingatiwa kuwa Tekashi 69 ana bifu na marapa hao wawili.