You are currently viewing Tekno Miles atangaza kuacha bangi

Tekno Miles atangaza kuacha bangi

Hitmaker wa “Go”, Msanii Tekno Miles amewashangaza wengi baada ya kusema kwamba ameamua kuacha kabisa matumizi ya bangi.

Kupitia video aliyochapisha kwenye mitandao yake ya kijamii, Tekno anasema kuwa alifikia uamuzi huo na hadi juzi alikuwa tayari amemaliza zaidi ya saa 48 sawa na siku mbili bila kutumia marijuana.

Msanii huyo kutoka Nigeria anasema kuwa awali hangeweza kukaa bila kutumia bangi hata usiku mmoja, lakini sasa haamini kama kweli ameweza kukaa zaidi ya saa 48 pasi na kukaribia bangi.

“Huyu ni mimi, saa 48 baadaye au tuseme zaidi ya saa hizo, bila bangi, bila marijuana, ninapenda jinsi ninavyoendelea nilipata japo kulala kiasi usiku. Ndiyo huyu mimi niko vizuri, macho yangu sasa yako vizuri hayana zile dalili za kuonesha utumizi wa vileo. Najua itakuwa vizuri hata zaidi,” anasema Tekno

Tekno si msanii wa kwanza kuweka wazi kuwa amekuwa akitumia dawa za kulevya kwa ajili ya kumpa mihemko ya kufanya ngoma kali ambazo huwa na mapokezi makubwa kwa mashabiki wake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke