You are currently viewing TEMS APATWA NA TATIZO LA KOO

TEMS APATWA NA TATIZO LA KOO

Mwimbaji nyota wa muziki kutoka Nigeria tems ambaye anafanya vizuri Kimataifa ameweka wazi kukutwa na tatizo la koo ambalo limepelekea kutotokwa na sauti.

TEMS ametangaza hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo kwenye taarifa yake ameeleza kwasasa hayupo sawa kufuatia kupata tatizo hilo. Hivyo inamlazimu kusimama kufanya muziki kwa muda, pamoja na kusitisha matamasha yake mawili aliyokuwa akitarajia kuyafanya huko Birmngham na London nchini Uingereza.

Itakumbukwa tatizo hilo la sauti pia liliwahi kumkuta mwimbaji na mtayarishaji wa muziki nchini nigeria Tekno mwaka 2018, ambaye yeye alipumzika kwa takribani mwaka mmoja na nusu hadi kuwa sawa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke