You are currently viewing TEMS ASHINDA TUZO YA BEST INTERNATIONAL ACT BET 2022

TEMS ASHINDA TUZO YA BEST INTERNATIONAL ACT BET 2022

Mwanamuziki wa Nigeria, Tems ameshinda tuzo ya BET 2022 katika kipengele cha Best International Act katika tuzo hizo zilizotolewa usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Microsoft Theater Jijini Los Angeles, Marekani.

Tuzo hizi zinaandaliwa na Black Entertainment Television (BET) toka Juni 19, 2001 zinalenga kusheherekea mafanikio ya kazi za Wamarekani Weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji na michezo.

Tems alikuwa anawania kipengele hicho na Drave (UK), Dinos (Ufaransa), Fally Ipupa (DR Congo), Fireboy DML (Nigeria), Little Simz (UK), Ludmilla (Brazil), Major League DJZ (Afrika Kusini) na Tayc (Ufaransa),

Ikumbukwe toka mwaka 2019 hadi 2021, Burna Boy wa Nigeria ameibuka mshindi mfululizo na kumfanya kutambulika kama msanii aliyeshinda mara nyingi kwenye kipengele cha Best International Act ambacho BET walikianzisha mwaka 2010 kikijulikana kama cha Best International Act: Africa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke