You are currently viewing TETESI ZA RIHANNA NA ASAP ROCKY ZASHIKA KASI MTANDAONI

TETESI ZA RIHANNA NA ASAP ROCKY ZASHIKA KASI MTANDAONI

Tetesi kutoka nchini Marekani zinaeleza kuwa mwanamuziki Rihanna amechana na mpenzi wake Asap Rock ambaye ndio baba mtoto wake mtarajiwa.

Inadaiwa kuwa hii imetokana na Rihanna kumfumania mpenzi wake huyo akimsaliti na mmoja wa wabunifu wa viatu kutoka katika kampuni ya Fenty aitwaye Amina Mauddi.

Tetesi hizo zinasema Asap Rocky na Amina Muaddi walianza mahusiano tangu mwezi Februari mwaka huu kwenye maonesho ya Paris Fashion Week.

Taarifa hiyo imeenea kwa kasi kote mitandaoni haswa katika mtandao wa twitter baada ya mtumiaji mmoja wa mtandao huo kuvujisha taarifa hiyo.

Jambo lililoifanya idadi kubwa ya mashabiki na wafuatiliaji wa wapenzi hao kuanza kutiririsha maoni mbalimbali kuhusu jambo hilo. Baadhi ya vyanzo vimeonesha kuwa huenda kukawa na ukweli wa fununu hizi.

Rihanna na Asap Rock siku za hivi karibuni wamekuwa wakiingia kwenye trending kama moja ya wapenzi wenye kuvutia zaidi baada ya wawili hao kuweka bayana kuwa wanatarajia kupata mtoto siku za usoni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke