Rapa The Game kutoka Marekani amefunguka kuhusu biashara yake ya muziki wa rap pamoja na ukaribu wake na Kanye West kwenye Episode mpya ya Drinks Champs inayotarajia kutoka Alhamisi hii
The Game amesema kuwa ukaribu wake na kanye west katika wiki mbili zilizopita umemsaidia vitu vingi kama kazi zake za muziki, kuongelewa sana mitandaoni kuliko hata alivyowahi kuwa karibu na Dre.
Kauli ya The Game imekuja mara baada ya Dr. Dre kutompa nafasi kwenye onesho la Super Bowl 2022 wiki kadhaa zilizopita, jambo ambalo lilionekana kumkera sana rapa huyo ikizingatiwa kuwa amefanya kazi na Dre kwa muda kwenye lebo ya muziki ya Aftermath Records.