You are currently viewing THE GAME ADAI YEYE NDIYE RAPA BORA KULIKO EMINEM

THE GAME ADAI YEYE NDIYE RAPA BORA KULIKO EMINEM

Rapa kutoka Marekani The Game anaendelea kusisitiza kuwa yeye ni rapa bora kuliko Eminem.

Kupitia podcast ya All the Smoke, The Game amesema kwamba Eminem ni Mwandishi mzuri lakini yeye ni bora kumliko Eminem.

Sababu kuu ya The Game kufunguka hayo ni kwamba anaamini Eminem ni mkali wa kuandika na kuchana lakini muziki wake sio mkubwa kutokana na kutochezwa kwenye kumbi za starehe na mtaani, ambapo yeye amefanikwa kwa hilo.

The Game ameendelea kufunguka kwamba wadau wa muziki hawakuwekeza hela kwenye muziki wake na hakupata support ambayo Eminem na 50 Cent wameipata, kama wangefanya hivyo kwake basi ingekuwa habari nyingine.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke