Rapa kutoka Marekani The Game amekanusha taarifa zote ambazo zinadai kwamba alimtukana Jay-Z baada ya kumnyima nafasi ya kutumbuiza kwenye Halftime show ya Super Bowl 2022.
Kupitia instagram page yake The Game amesema hana mtu yeyote wa kumsemea isipokuwa yeye mwenyewe. Hii imekuja kufuatia meneja wake Wack 100 kufunguka kwamba The Game alimtukana Jay-Z tusi zito “Suck My D*k” baada ya kunyimwa nafasi hiyo ya kutumbuiza.
The Game anasema hakuzungumza na mtu yeyote kuhusu Jay-Z au show ya Super Bowl, na kwa upande wake ilikuwa ni show nzuri sana.
Rapa huyo alienda mbali zaidi na kumsifia Jay-Z kwa kazi nzuri ya kuendelea kufungua milango, na ameahidi kumuunga mkono kwa kila kitu.