You are currently viewing THE GAME NA TIMU YAKE WAKASIRIKA, WAHOJI NI KWANINI DR. DRE ALIMCHAGUA 50 CENT KWENYE SUPER BOWL 2022

THE GAME NA TIMU YAKE WAKASIRIKA, WAHOJI NI KWANINI DR. DRE ALIMCHAGUA 50 CENT KWENYE SUPER BOWL 2022

Stori kubwa wiki hii kwenye burudani ni Super Bowl Half Time Show ambayo inatajwa kuwa ya kihistoria, lakini The Game ana malalamiko yake.

Baada ya 50 Cent kupandishwa na kutumbuiza kama Guest Artist, Rapa The Game pamoja na timu yake wameonekana kutopenda uamuzi huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, The Game ame-share ujumbe uliowekwa na miongoni mwa memba kwenye timu yake, ambao unasema inakuaje wanampa 50 Cent hiyo nafasi na sio The Game? Game alistahili kuwepo kwenye Jukwaa hilo pia

Kauli ya The Game imekuja mara baada ya Super Bowl 2022 Halftime Show kufunguliwa kwa perfomance ya Dr. Dre na Snoop Dogg kupitia ngoma ya “The Next Episode” na “California Love” ya Tupac Shakur, ambapo Rapa na mfanyabiashara 50 Cent alitokea kwenye dakika ya 3:10 kupiga performance ya kufa mtu na ngoma ya “In Da Club” na kuamsha shangwe la aina yake.

Eminem ndiye alimpa mashavu 50 Cent kutumbuiza kwenye halftime ya Super Bowl 2022. Eminem ndiye alitoa wazo hilo na kupitishwa na Dre pamoja na wote ambao walikuwa kwenye orodha ya watumbuizaji rasmi.

Ikumbukwe Mtayarishaji mkongwe  kutoka Marekani Dr. Dre alitumia shillingi millioni 795 za Kenya kwa ajili ya kutayarisha performance nzima ya Halftime kwenye fainali za Super Bowl 2022 zilizofanyika Februari 14 katika uga wa SoFi huko California.

Dunia ilishuhudia Dr. Dre akiandika historia akiwa na wakali wa Hip Hop nchini Marekani; kama Kendrick Lamar, Snoop Dogg, Eminem, 50 Cent na mwanadada Mary J Bridge.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke