Mwanamuziki kutoka Canda The Weeknd ndiye Mwanamfalme wa Pop kwa sasa duniani.
Msanii huyo amempindua Justin Bieber kwa kufikisha jumla ya wasikilizaji wa mwezi milioni 85.86 kwenye mtandao wa Spotify akimuangusha Justin bieber mwenye wasikilizaji milioni 83.86
Justin Bieber alikuwa amekalia kiti hicho kwa siku 190 mfululizo na kusimikwa taji la Prince of Pop.
The Weeknd anaendelea kufanya vizuri na album yake mpya “Dawn FM” ambayo hadi sasa imesikilizwa zaidi ya mara milioni 750 kwenye Spotify.