You are currently viewing TIKTOK KUJA NA SOFTWARE MAALUM YA KURUSHA LIVE EVENTS KUPITIA KOMPYUTA

TIKTOK KUJA NA SOFTWARE MAALUM YA KURUSHA LIVE EVENTS KUPITIA KOMPYUTA

TikTok inafanya majaribio ya software maalum ya Desktops (Computers) ambayo itawezesha watumiaji kurusha LIVE Events moja kwa moja katika Desktops.

TikTok Live Studio itakuwa ni maalum kwa matumizi ya Live Streaming zote za TikTok na watumiaji wataweza kuitumia katika kurusha matukio ya Live kutoka katika Computer kwenda katika simu na platform yote ya TikTok.

Wakati apps nyingine zinajaribu kuwa kama TikTok, TikTok inazidi kuongeza ukubwa wake na kuwa kama Twitch, YouTube, na Facebook Gaming.

TikTok Live Studio itakuwa ni maalum kwa Gamers, kampuni za kurusha matukio ya LIVE, Shughuli kubwa za Events na Live Streams za TikTok. Kwa software hii unaweza kurusha events live, kuweka captions, ku-mix nyimbo na audios, kusoma comments, kujibu watu, na unaweza ku-mix inputs za simu, Moxer na computer kwa pamoja.

Software hii imeanza rasmi kama sehemu ya majaribio kwa baadhi ya maeneo; inaonyesha TikTok inaweka focus ya kuwa kubwa zaidi ya kuwa short video platform. Kwa feature hii, itakuwa inashindana na Twitch, YouTube Games na Facebook Games ambazo zimekuwa zikiweka Live Streaming kwa ukubwa, hasa kwa kulenga soko la Gamers.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke