TikTok imeanza kupatikana rasmi katika TV zote za LG ambazo zinatumia mfumo wa webOS 5.0 na kuendelea. Hii itasaidia kuweka urahisi kwa watumiaji wa TV kuona videos fupi za TikTok katika TV.
Mwaka huu hatua kubwa ambayo mtandao wa TikTok ni kuchukua soko la Smart TV.
Tayari ilitoa app kwa watumiaji wa Android TV na mwezi huu imeongeza upatikanaji wake kwa watumiaji wa webOS.
Ni mpango mzuri kama ilivyo katika Netflix na YouTube zilivyofanikiwa kuwa na apps katika smart TV.