Timu ya kampeni ya Kanye West imetoa madai ya kuibiwa kiasi kikubwa cha pesa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2020, kwa njia za ulaghai.
Kiasi cha pesa kilichoibiwa na mtu ambaye hakuwa kwenye team hiyo ya kampeni ya kanye west kimetajwa ni zaidi ya shilingi laki 4 za Kenya.
Fedha hizo zilikuwa zikiibwa kuanzia Disemba mwaka wa 2020 hadi Februari mwaka wa 2021 katika akaunti ya Kanye West iliyopo katika First Bank of Wyoming.
Kanye West ambaye alikuwa akiwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu mwaka wa 2020 nchini Marekani alishindwa lakini hivi karibuni kwenye moja ya mahojiano yake ameahidi kuwania tena kiti hicho cha urais mwaka wa 2024.