Malkia wa umbea nchini Uganda Tinah Fierce amefunguka na kusema msanii Spice Diana hajui kabisa kupendeza kwani mara nyingi hata nguo anazovaa ni kama zimetundikwa tu mwilini mwake.
Tinah Fierce anasema wapo watu wengine wana pesa nyingi nchini Uganda lakini suala la kuvaa kwao ni zero na kumtolea mfano Spice Diana kuwa ni moja ya watu ambao hajui kuvaa na hata nguo akivaa zinakuwa hazimkai vizuri mwilini
Kupitia kipindi chake cha Random Thoughts ambacho kinaruka kupitia mtandao wa Youtube Tinah amemsuta vikali Spice Diana kwa hatua ya kuvaa nguo za bei nafuu kutoka Uchina, na bila aibu ku-share picha zake akiwa amevali nguo hizo kwenye mitandao ya kijamii.
Malkia huyo wa umbea ameenda mbali zaidi na kusema kwamba Spice Diana hapaswi kulalamika juu ya Tuzo za Janzi ikizingatiwa kuwa huwa hazungumzi kuhusu mambo mengine ambayo yanawaathiri watu wa kawaida.
“Lala tu na uendelee kuvaa nguo zako za bandia na bei rahisi,” Tinah alisema.
Ikumbukwe Tinah Fierce alifutwa kazi Urban TV kutokana na tabia yake ya kuwashambulizi watu maarufu nchini Uganda lakini sasa hivi chaneli yake ya YouTube inampa uhuru wa kuzungumza chochote