Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Tip Swizzy anaendelea kutupasha mpya kuhusu maisha yake chini ya lebo ya muziki ya Big Talent Entertainment inayomilikwa na Eddy Kenzo.
Tip swizzy anasema anajutia kufanya kazi lebo hiyo kwa sababu hakufaidika na muziki wake. Msanii huyo amesema Eddy kenzo alimnyanyasa kwa kumlipa malipo duni licha ya kwamba alitumbuiza kwenye matamasha mengi ya muziki nchini Uganda.
Kulingana na tippy swizzy kuondeka kwake kwenye lebo ya Big Talent Entertainment kumsaidia kukua kimuziki na kiuchumi.
Ikumbukwe mwaka wa 2016 Tippy swizzy aligura lebo ya Big Talent Entertainment baada ya kuingia kwenye ugomvi na bosi wa lebo hiyo Eddy Kenzo kutokana na ishu ya malipo.