Staa wa muziki kutoka Nigeria, msanii Tiwa Savage yupo mbioni kuweka historia kupitia ziara yake ya kimuziki iitwayo Water & Garri Tour atakayoifanya kwenye miji iliyopo Kaskazini mwa Marekani.
Hitmaker huyo wa ‘Somebody’s Son’ ametaja ziara hiyo kuanza Mei 15 huko jijini New York na itafanyika ndani ya miji 17 kwa kipindi cha miezi miwili.
Tiwa Savage ambaye anatarajiwa baadae mwaka huu kuachia albamu yake mpya, ziara hiyo inakuwa ziara kubwa na ya kwanza kwake kuifanya Marekani.