Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, msanii Tiwa Savage amethibitisha kumalizika (sold out) kwa tiketi zote katika Show yake itayofanyika Juni 19, katika ukumbi wa Longboat huko Toronto, Canada.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Tiwa Savage ameandika ujumbe unaosomeka “We already sold out Toronto 💫💫💫💫 #WaterAndGarriTour. Ticket link for other cities in my bio ❤,”
Show hiyo iliyopo ndani ya ziara yake ya Water & Garri itaanza rasmi Mei 15 huko jijini New York na itafanyika ndani ya miji 17 kwa kipindi cha miezi miwili.
Hitmaker huyo wa ‘Somebod’s Son’ Tiwa Savage ambaye baadae mwaka huu anatarajiwa kuachia albamu yake mpya, ziara hii inakuwa ni ziara kubwa na ya kwanza kwake.