Rapa Tory Lanez, amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya mahakama kumpata na hatia kwenye shtaka la kumpiga risasi Megan Thee Stallion, Julai mwaka 2020.
Kwa mujibu wa L.A Times, rapa huyo amekaririwa akisema kuwa amesikitishwa na uamuzi wa mahakama lakini anaamini kila jambo katika maisha lina sababu zake.
Tory Lanez atabaki rumande akingoja hukumu yake kusomwa Januari 27, mwaka 2023 baada ya kukutwa na hatia kwenye mashtaka matatu ikiwemo kumshambulia Megan kwa kutumia silaha lakini pia kubeba silaha iliyopakiwa risasi na ambayo pia haijasajiliwa.
Hata hivyo timu ya Tory Lanez imeonekana kutoridhishwa na maamuzi ya mahakama, hivyo wakili wake George Mgdesyan anapanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo kwani hakuna ushahidi uliojitosheleza.