Mwanamuziki kutoka Marekani August Alsina amedai kwamba amepigwa na kuumizwa vibaya na Tory Lanez.
Kwa mujibu wa andiko lake kwenye mtandao wa instagram, Alsina amesema Tory alimshambulia wakati akiondoka kwenye onesho moja mjini Chicago Juzi Jumamosi.
Jana Jumapili mwimbaji huyo wa R&B ali-posti picha ambazo zinamuonesha akivuja damu mdomoni na kuelezea tukio hilo kwamba Lanez alimfuata akiwa na walinzi 8 huku yeye akiwa hana ulinzi wowote.
Kwenye maelezo yake, Alsina anasema alishambuliwa na Tory Lanez baada ya kutompa mkono kama ishara ya kusalimiana kwa kuwa alifuata masharti ya madaktari wake kutopeana mikono kiholela.
Tory Lanez naye amejibu kwa kukanusha taarifa hizo ambapo kupitia insta story yake, amedai siku hiyo hakuwepo eneo hilo na alikuwa studio akifanya kazi zake.