Mahakama ya jiji la Los Angeles imemkuta na hatia rapa Tory Lanez kwa makosa matatu ikiwemo la kumshambulia na kumjeruhi kwa risasi aliekuwa mpenzi wake mwanamuziki Megan Thee Stallion.
Tukio hilo lilitokea baada ya mabishano yaliyosababishwa na utani ambapo inadaiwa Tory Lanez alikasirika na kufyatua risasi zilizomjeruhi miguuni Megan Thee Stallion.
Mara baada ya maamuzi ya mahakama Lanez aliondoka mahamani hapo chini ya ulinzi mkali kuelekea gereza la Los Angeles kusubiri kuanza kutumikia adhabu yake.
Tory Lanez ambaye jina lake ni Daystar Peterson anaweza kuhukumiwa kifungo cha mpaka miaka 22 jela katika hukumu inayotarajiwa kusomwa Januari 25.