Mwaka mmoja baada ya kukanusha mashtaka ya kumpiga risasi Megan Thee Stallion, Mwanamuziki Tory Lanez amegoma kuingia makubaliano na waendesha mashtaka kwenye shauri hilo ambalo Tory anadaiwa kumpiga risasi mbili za mguu Megan Thee Stallion mwezi Julai mwaka wa 2020.
Kwa mujibu wa Rolling Stone, Tory Lanez atatakiwa kufika mahakamani Disemba 14, 2021 kutoa ushuhuda wake moja kwa moja ya kile kilichotokea usiku huo wa Julai 12 mwaka wa 2020. Kama akikutwa na hatia, Tory Lanez atahukumiwa kifungo cha miaka 23 Jela.