Rapa kutoka nchini Marekani Travis Scott ameondolewa kwenye orodha ya watumbuizaji wa tamasha la Coachella kwa mwaka 2022 kufuatia tukio la vifo vya watu 10 kwenye tamasha lake Astroworld Festival mwezi November mwaka huu.
Hii imekuja mara baada ya watu kuleta mapingamizi mtandaoni wakitaka rapa huyo kuondolewa kwenye orodha ya watumbuizaji, mapingamizi ambayo yalifikia saini 60,000.
Ikumbukwe Tamasha la Astroworld Festival ambalo liliandaliwa na Travis Scott kwa lengo kusaidia elimu kwa vijana wadogo, lilikumbwa na simanzi mara baada ya watu takribani 11 kufariki dunia na wengine kujeruhiwa wakati onesho hilo likiendelea, hivyo kupelekea kuahirishwa.