Rapa kutoka Marekani Travis Scott na Baby Mama wake Kylie Jenner wanapanga kubadilisha Jina la mtoto wao wa kiume (Wolf Webster), wawili hao wanajuta kumpatia Jina hilo mtoto huyo wa pili ambaye ana umri wa miezi 8 sasa.
Kwa mujibu wa Kylie kwenye Episode ya Keeping Up with The Kardashians, Jina hilo lilitolewa na Khloe Kardashian na kwa wakati huo alilipenda lakini punde tu baada ya kuliandika na kuangusha saini kwenye cheti cha Kuzaliwa, aliingia majuto ya kutamani kulibadilisha.