Mwanamuziki kutoka Marekani Trey Songz anazidi kuandamwa na tuhuma za udhalilishaji baada ya tuhuma ya ubakaji pamoja na unyanyasaji wa kingono zilizotoka Februari mwaka huu, sasa limeibuka shtaka lingine jipya dhidi yake.
Kwa mujibu wa TMZ, mwimbaji huyo maarufu duniani kwasasa anadaiwa fidia kwa tukio alilolifanya mwaka 2013 baada ya video ya tukio hilo kusambaa hivi karibuni. Trey Songz kwenye video hiyo anaonekana kulitoa nje titi la mwanamke mmoja aliyehudhuria party ambayo yeye (Trey Songz) ndiye alikuwa host wa party hiyo iliyofanyika kwenye casino la Foxwoods Resort huko Ledyard.
Mwanamke huyo alietambulika kwa jina la Megan Johnson sasa anataka fidia ya mamilioni ya pesa, anadai fidia ya $5 Milioni. Barua kutoka kwa mawakili wa Megan Johnson, Trey Songz anatuhumiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia na kupuuza usalama wake bila kujali.
Kwenye maelezo yake Megan Johnson amedai kuwa alikuwa amemuomba rafiki yake ampige picha Trey Songz alipokuwa nyuma yake ndipo Trey alipomshika na kufanya kitendo hicho cha udhalilishaji.