You are currently viewing TREY SONGZ KWENYE TUHUMA NYINGINE YA UBAKAJI, ADAIWA KUMUINGILIA KINYUME NA MAUMBILE MWANAMKE MMOJA

TREY SONGZ KWENYE TUHUMA NYINGINE YA UBAKAJI, ADAIWA KUMUINGILIA KINYUME NA MAUMBILE MWANAMKE MMOJA

Staa wa muziki kutoka nchini Marekani Trey Songz anazidi kuandamwa na tuhuma za ubakaji pamoja na unyanyasaji wa kingono, mwanamke wa tatu amejitokeza na kudai fidia ya shilling billion 2.3 za Kenya  kwa madai ya kubakwa na kuingiliwa kinyume na maumbile.

Kwa mujibu wa TMZ, shauri hilo lilifunguliwa Februari 15 mwaka huu ambapo mwanamke huyo alisema Trey Songz alimwalika kwenye party katika nyumba moja mjini Los Angeles, baadaye alimpeleka chumbani wakiwa na makubaliano ya kufanya mapenzi kawaida.

Walipofika chumbani, Trey Songz alimsukuma chini na kuanza kumlazimisha kumuingilia kinyume na maumbile, baada ya kupambana kujioka kwenye mikono ya mkali huyo wa R&B, mwanamke huyo anasema alizidiwa nguvu na Trey songz na hivyo akamuingilia kinyume na maumbile kwa nguvu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke