Staa mpya wa muziki nchini Trio Mio ameingia ubia wa kufanya kazi na Darasa Afrika jukwaa la kutoa mafunzo kwa wanafunzi mtandaoni.
Trio Mio ametengaza habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram huku akieleza kuwa ana furaha kujiunga na familia ya Darasa Afrika.
Hitmaker huyo wa “Steppa” amewataka wanafunzi walio kwenye likizo kuendeleza masomo yao mtandaoni kupitia jukwaa la Darasa Afrika wakati huu shule zimefungwa.
Kwa sasa Trio Mio atatakiwa kutangaza huduma za Darassa Afrika kwa mashabiki zake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuiongeza jukwaa hiyo wanafunzi watakaopata maarifa kupitia masomo wanayotoa kwa njia ya mtandao.