You are currently viewing TRIO MIO AKANUSHA KUPATA D+ KWENYE MTIHANI WA KITAIFA WA KCSE

TRIO MIO AKANUSHA KUPATA D+ KWENYE MTIHANI WA KITAIFA WA KCSE

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya Trio Mio amekanusha tetesi zinazosambaa mtandaoni kuwa alipata alama D+ kwenye mtihani wa kitaifa wa KCSE wa mwaka wa 2021.

Katika mahojiano ya hivi karibuni Trio Mio amesema madai hayo hayana ukweli wowote kwa kuwa bado anaendelea na masomo yake ya Shule ya upili.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Step” amepulizia mbali madai ya kusomea nyumbani kwa  kusema kwamba bado anasomea shule za bweni.

Kauli yake imekuja mara baada ya watu kusambaza uvumi mtandaoni kuwa msanii huyo amepata alama ya D+  pindi tu waziri wa elimu Prof. George Magoha alipotangaza matokea ya mtihani wa kitaifa wa KCSE mwaka wa 2021

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke